NEWS

Thursday 17 December 2020

Mugumu kuanza kupata maji safi mapema mwakani

Mkurugenzi Mtendaji wa MUWASA, CPA Joyce Msiru akizungumza na Mara Online News ofisini kwake, hivi karibuni.

 

WAKAZI wa Mji wa Mgugumu na vijiji jirani katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara, wataanza kupata maji safi na salama baada ya ujenzi wa chujio la maji katika bwawa la Manchira kukamilika Februari 2021.

 

“Tumeanza kusimamia ujenzi wa chujio hilo Oktoba mwaka huu [2020] kwa kutumia Force Account,” Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), CPA Joyce Msiru, ameiambia Mara Online News ofisini kwake, hivi karibuni.

 

Hivi karibuni, CPA Msiru amefanya ziara ya kukagua mradi huo na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wake - lengo likiwa ni kuboresha huduma ya maji kwa wananchi.

 

 “Nimekuwa Serengeti kukagua miradi ya maji vijijini inayosimamiwa na MUWASA na maendeleo ni mazuri,” amesema.

Mradi wa ujenzi wa chujio la maji katika bwawa la Manchira.

 

Mbali na chujio la maji katika bwawa la Manchira, CPA Msiru amekagua mradi wa Kitunguruma, yote hiyo ikigharimiwa na Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

 

Mwenyeji wa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MUWASA katika ziara hiyo amekuwa Meneja Mradi, Mhandisi Lucas Kivegalo. 

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages