MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, amewahimiza wananchi kuiunga mkono kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kutumia huduma zake zikiwemo za kifedha na internet.
Mbunge Ghati ameyasema hayo mara baada ya kukata utepe wa uzinduzi wa duka la Airtel mjini Musoma, leo Januari 7, 2021.
“Tuiunge mkono kampuni ya Airtel kwani wamejipanga kuinua uchumi wa mkoa wa Mara na nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla, na huduma zao ni nzuri,” amesema Ghati na kuupongeza uongozi wa Airtel kwa kuwasogezea wana-Mara huduma karibu.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (kushoto), akionesha kifaa cha 4G ya internet ya Airtel yenye kasi zaidi. Kulia ni Afisa Mauzo wa Airtel Musoma, Leonard Maige.
Awali, Afisa Mauzo wa Airtel Musoma, Leonard Maige, amesema lengo kuu la kufungua duka hilo ni kuwezesha wateja wake na wananchi kwa ujumla kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo kwa urahisi.
Maige ametaja huduma hizo kuwa ni pamoja na za kifedha, internet, usajili wa laini, urejeshaji wa laini zilizopotea na kuunganishiwa 4G kwa ajili ya internet yenye kasi zaidi.
(Habari na picha zote na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment