NEWS

Saturday, 15 November 2025

Mara Online wapokea ‘kits’ za Serengeti Safari Marathon 2025, zimo t-shirts



Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon, Timothy Mdinka, akimakbidhi Mwakilishi wa Mara Online, Judith Juma, ‘kits’ za washiriki wa mbio hizo kwa mwaka 2025.

Na Mwandishi Wetu
Mwanza
--------------

Mara Online wamepokea ‘kits’ za washiriki wa mbio za Serengeti Safari Marathon zitakazofanyika Novemba 29, 2025.

Kama ilivyo kawaida, mbio hizo ambazo huandaliwa kila mwaka, zitafanyika katika eneo la lango la Ndabaka ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Mkurugenzi wa Serengeti Safari Marathon, Timothy Mdinka, alikabidhi’ kits’ hizo kwa Mwakilishi wa Mara Online, Judith Juma, jijini Mwanza jana.

“Tayari tumepokea mzigo wa kutosha, zikiwemo t-shirts nzuri na zenye ubora, tunawakaribisha wana-Mara na wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa ujumla kujisajili kushiriki mbio bora kabisa ambazo hufanyika ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti,” alisema Judith.

Serengeti Safari Marathon huvutia mamia ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchi, huku zikibeba kaulimbiu zinazohamasisha uhifadhi wa mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages