NEWS

Friday 1 January 2021

Naibu Waziri Waitara atumia Sikukuu ya Mwaka Mpya kushiriki usafishaji mazingira soko la Sirari

 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) akizoa uchafu katika jalala la Sirari, leo mchana.

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mwita Waiatra, leo Januari 1, 2021 amekwenda kukagua utekelezaji wa agizo lake la kuondoa marundo ya uchafu  yaliyokithiri katika soko la mji mdogo wa Sirari, wilayani Tarime Mara.

 

"Agizo langu liko palepale kuwa lazima huu uchafu oundoke eneo hili," Waitara amesisitiza alipowasili katika eneo hilo leo mchana.

 

Waitara ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini, amekuta kazi ya kuondoa takataka hizo ikiendelea, ambapo na yeye ameungana na wengine kushika koleo na kuzoa sehemu uchafu huo.


Naibu Waziri Waitara akiendelea kuzoa uchafu katika jalala la soko la Sirari.

Naibu Waziri huyo ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) kutafuta sehemu nyingine dampo ambalo halitahatarisha afya za wananchi kama ilivyo kwa sasa.

 

Jana Alhamisi, Waitara amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Tarime na kuagiza Mkurugenzi Mtendaji, Apoo Castro Tindwa na Afisa Mazingira wa Halmashauri hiyo, Martha Mahule kutumia Sikukuu ya Mwaka Mpya 2021 kufanya usafi wa kuondoa takataka katika soko la Sirari.

Naibu Waziri Waitara akisisitiza jambo baada ya kukagua shughuli ya usafi inayooendelea katika soko la Sirari. Wa kwanza kushoto ni Diwani wa Kata ya Sirari, Amos Sagara.

Mkurugenzi Mtendaji, Tindwa na Afisa Mazingira, Mahule, wamefika katika soko hilo kusimamia usafi, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu vya Sirari.

 

Waitara ametoa agizo kwa halmshauri zote nchini kuwa na maeneo maalumu ya kutupa takataka bila kuhatarisha afya za wananchi. 

 

(Habari na pichaa zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages