NEWS

Friday 29 January 2021

Wachina washtakiwa kushambulia, kudhalilisha mfanyakazi

Raia wa China wakizungumza na wakili wao (kulia) mahakamani Musoma mkoani Mara walikofikishwa jana Januari 28, 2021 wakishtakiwa kumshambulia na kumdhalilisha mfanyakazi.

RAIA wa China, Cai Liang Lan, Yun Nsung na Zhang Yun Lin - wanaofanya kazi kampuni ya Unik Engineering Construction Lesotho inayoendesha mradi wa maji Mugango, Kiabakari wilayani Musoma, Mara, wamefikishwa mahakamani wakishtakiwa kumshambulia na kumdhalilisha mfanyakazi.

 

Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Tumaini Marwa jana Januari 28, 2021, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Frank Nchamila amedai kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo katika mtaa wa Kusaga, Desemba 22, 2020.

 

Nchamila amesema kosa kwanza ni la kumshambulia na kumsababishia maumivu ya mwili, Melinda Franko na kosa la pili ni la kumdhalilisha kijinsia.

 

Amesema washtakiwa hao walitenda makosa hayo kinyume na vifungu vya Sheria Na. 138 na 241 kinyume na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

 

Baada ya kusomewa mashitaka hayo washitakiwa hao wamekana makosa hayo na kuachiwa kwa dhamana, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Februari 4, 2021.

 

(Imeandikwa na Shomari Binda, Musoma)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages