NEWS

Wednesday 3 February 2021

Mshindi Tuzo ya Mkulima Bora wa Kahawa atinga Sauti ya Mara

Mkulima bora wa kahawa, Steven Mwita Marko

MSHINDI wa tuzo mbili za ukulima bora wa kahawa, Steven Mwita Marko, leo Februari 3, 2021 ametembelea ofisi za gazeti la Sauti ya Mara mjini Tarime na kueleza mengi ya kusisimua kuhusu kilimo cha zao hilo la biashara.

 

Gazeti la Sauti ya Mara ni chombo dada cha habari cha blogu hii ya Mara Online News, vyote vikiwa vimejikita katika kuandika habari za maendeleo na uhifadhi - zinazokidhi mahitaji ya jamii nzima.

 

Marko, mkulima wa kahawa aina ya Arabica na mkazi wa kijiji cha Nyantira kilichopo wilaya ya Tarime mkoani Mara, alishinda tuzo ya kwanza ya mkulima bora wa kahawa kanda ya uzalishaji ya Mara katika Maonesho ya Kilimo (Nanenane) mkoani Dodoma mwaka 2013.

Kahawa

Marko alikabidhiwa tuzo ya pili ya mshindi wa kwanza wa ukulima bora wa kahawa Agosti 8, 2020 kwenye Maonesho ya 28 ya Nanenane yaliyofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

 

Makala maalumu ya mahojiano ya kina na mkulima huyo yatachapishwa kwenye toleo la Sauti ya Mara Jumatatu Februari 8, 2020.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages