NEWS

Monday 15 February 2021

TRA yaomba watendaji kata kusaidia kukomesha magendo mpaka wa Sirari

Afisa Mkuu wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Valentina Baltazar (aliyesimama) akizungumza katika kikao na maofisa watendaji wa kata.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewaomba maofisa watendaji wa kata kutoka Halmashauri za Tarime Mjini na Tarime Vijijini kuwa mabalozi wa kuwaelekeza wananchi kutumia mpaka rasmi wa Sirari ili kukomesha biashara za magendo mpkani kwa kuwa zinaikosesha serikali mapato.

 

Hayo yamesemwa jana Februari 15, 2021 na Afisa Mkuu wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Valentina Baltazar, wakati akizungumza na watendaji hao katika kikao cha kuwajengea uwezo wa kuzifahamu taratibu za kiforodha za kufuata wakati wa kuingiza na kutoa mzigo katika mpaka wa Sirari mjini Tarime Mkoani Mara.

Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Mwandamizi wa TRA Mkoa wa Mara, Zake Wilbard Rwiza, akizungumza katika kikao hicho.


#MaraOnlineNews-Updates

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages