NEWS

Sunday 7 March 2021

Kikundi cha ITY chaadhimisha Siku ya Wanawake kwa kusaidia watoto wenye mahitaji Tarime

Kikundi cha wanawake cha Itambue Thamani Yako (ITY) kikikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji wanaolelewa katika kituo cha Angel House wilayani Tarime, Mara, leo.

KIKUNDI cha wanawake cha Itambue Thamani Yako (ITY) kilichopo Tarime mkoani Mara, leo Machi 7, 2021 kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kukabidhi misaada mbalimbali katika kituo kulea watoto yatima cha Angel House kilichpo Gamasara, nje kidogo ya mji wa Tarime.

 

Misaada iliyokabidhwa kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho ni pamoja mchele, sukari, mafuta ya kula, sabuni na vinywaji.

Picha ya pamoja wakati wa makabidhiano hayo.
 

Kiongozi wa kikundi hicho, Bibiana Alpheus amesema wamejipanga kufanya kazi kubwa ya kuwezesha wanawake wa Tarime kutambua thamani na mchango kwa maendeleo katika jamii.

 

Mlezi wa watoto wa kituo cha Angel House, Anna Chacha ameshukuru kikundi hicho cha ITY kwa kuona umuhimu wa kusadia watoto wenye mahitaji.

Picha nyingine ya pamoja.
 

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Veronica Gabriel Marengo amepongeza ITY akisema ni mfano mzuri katika kuchochea maendeleo ya wanawake wilayani Tarime.

 

Aidha, Veronica amesema suala la elimu pia ni muhimu katika kuwafanya wanawake kutambua haki zao.

 

Awali, wanawake hao walifanya maandamano ya amani kuanzia kituo cha mafuta cha PKM kilichopo eneo la Rebu hadi Buhemba, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wakisisitiza suala umoja.

Wakiwa katika maandamano ya amani.
Maandamano yakiendelea.

SIku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka, ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaha huu wa 2021 inasema “Wanawake katika Uongozi: Chachu ya Kufikia Dunia yenye Usawa.”

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages