NEWS

Thursday 11 March 2021

UTAJIRI WA BINTI WA RAISI WA ZAMANI WA ANGOLA.

Isabel dos Santos (amezaliwa 1973) ni mfanyabiashara na mjasiriamali wa kike kutoka nchini Angola. Yeye ni mtoto wa kwanza wa rais wa zamani wa Angola José Eduardo dos Santos, ambaye alitawala nchi hiyo tangu mwaka 1979 hadi 2017.

 

Mnamo mwaka 2019 alitajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi kwenze bara la Afrika[6]. Mnamo 2013, kulingana na Forbes, jumla ya utajiri wake ilikuwa imezidi dolar za Kimarekani bilioni 2, hivyo alikuwa bilionea wa kwanza wa kike wa Afrika. Forbes alielezea jinsi dos Santos alivyopata utajiri wake kwa kuchukua hisa katika kampuni zinazofanya biashara nchini Angola, na kupendekeza kuwa utajiri wake unatokana kabisa na nguvu za kisiasa ya familia yake. [7] Mnamo Novemba 2015, BBC ilimtaja dos Santos kama mmoja wa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni.

 

Tangu mwaka 2018 serikali ya Angola ilikuwa ikijaribu kumshtaki Isabel dos Santos kwa jinai za ufisadi zilizochangia kwenye mzozo wa uchumi wa Angola katika miaka iliyotangulia. Lakini Isabel hakurudi tena Angola akibaki Ureno.

 

Mnamo Desemba 30, 2019, Mahakama ya Mkoa wa Luanda iliagiza kufungiwa kwa akaunti zake kwenye benki za Angola na kukamatwa kwa hisa zake katika kampuni pamoja na Unitel na Banco de Fomento Angola.  Tangu kuchunguliwa nchini Ureno pia amehamia UAE kama nchi yake rasmi ya kuishi.

 

Mnamo Januari 11, 2020, serikali ya Angola ilitangaza kwamba inachukua hatua za kisheria za kunyakua mali za dos Santos nchini Ureno.

Binti huyo amejijengea himaya yake kwa mapana na marefu na hasa katika mji mkuu Luanda ambao ni miongoni mwa miji ya kifakhari na ghali kabisa duniani.

Unapotembea katika mji mkuu wa Angola, Luanda, ni vigumu sana kushindwa kuitambua au kukumbana na alau kampuni moja ya Isabel Dos Santos.

 Binti huyo wa kwanza wa Rais Eduardo Dos Santos na ambaye ni mwanamke tajiri kabisa barani humo amejenga himaya yake ya utajiri katika moja ya miji ghali kabisa duniani -kutoka sekta ya mawasiliano, benki, televisheni ya satelaiti hadi kwenye spoti - kote huko anamiliki biashara kubwa zenye majina mjini Luanda.

Isabel anahodhi kampuni ya Unitel, ambayo ni kampuni kubwa kabisa ya simu za mkononi nchini Angola ikiwa na matawi 81 ndani ya mji huo mkuu pekee na zaidi ya wateja milioni 10 nchi nzima.

 Anamiliki msururu wa maduka makubwa, huku akiwa pia na hisa katika mabenki ya BIC na BFA sambamba na kampuni ya saruji ya Nova/ Cimangola.

Na kama haitoshi, mwanamama huyo anasimamia kampuni kubwa ya mafuta inayomilikiwa na serikali ya Sonangol pamoja na klabu ya soka ya Petro de Luanda inayofadhiliwa na kampuni yake.

 orodha ya utajiri wa Isabel Dos Santos ni ndefu ikijumuisha pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa nchini humo bila ya kuiweka kando sekta ya biashara ya madini, anasema mwanachama wa upinzani, Nelito Ekuikui:

''Tunaweza kuzungumzia pia sekta ya afya na uhusiano wake na kliniki kubwa kubwa za humu nchini bila ya kusahau sekta ya madini.

 Kampuni hizo  hazina ushindani. Hilo ni tatizo kubwa kwa nchi kwa sababu ni vigumu sana kwa wafanyabiashara wengine. Endapo tungekuwa na wafanyabiashara  wapya tungekuwa na nafasi nyingi za ajira.''

    



TASWIRA YA ISABEL KWA WAAFRIKA.

Baadhi ya watu wanamuangalia Isabel Dos Santos kama mfano wa wafanyabiashara barani Afrika ambao wametoa nafasi za ajira zinazohitajika kwa kiasi kikubwa, katika taifa ambalo asilimia 24 ya watu hawana kazi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014.

 

Lakini Nelito Ekuikui haliangalii suala hilo kwa jicho sawa na hilo. Yeye anasema utajiri wa Isabel na biashara zake nchini Angola hazina mpinzani na hilo ni tatizo.

Mwanaharakati wa Angola, Benmedoto Jeremias, anasema kwamba kuwa binti wa rais wa nchi kumemrahisishia mwanamama huyo shughuli zake zote ikilinganishwa na wawekezaji wengine, ''Kila kitu anachokimiliki Isabel Dos Santos kimetokana na upendeleo na fursa anazopata kutoka kwa baba yake.

Sio mali alizopata kwa juhudi zake''Kwa upande mwingine, mwandishi habari Rafael Marques ambaye amekuwa akifuatilia mzizi wa utajiri wa Isabel Dos Santos kwa kipindi cha miaka mingi, anasema kwamba baba yake, Jose Eduardo Dos Santos, amekuwa na dhima kubwa katika kumjengea utajiri huo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages