Wananchama wa MWEA Tawi la Nyanchabakenye, viongozi wa mashirika ya MWEA na OIKOS wakiwa katika warsha ya kubadilishana uzoezfu kijijini Nyanchabakenye, Roraya hivi karibuni. (Picha na Sauti ya Mara) |
WANACHAMA wa kikundi cha wanawake na vijana cha Nyanchabakenye kinachowezeshwa na Shirika la MWEA, wanatarajia kuanza kupata mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha kuendesha mradi wa kuweka na kukopa na mingine midogo midogo ya kujipatia kipato.
MWEA, yaani Mara Women Empowerment Assistance ni Shirika la lisilo la Serikali (NGO) - linalowezesha wanawake na vijana kupitia mikopo midogo midogo ili kuwawezesha kuondokana na maisha tegemezi.
“Kazi yetu kubwa ni kuwezesha wanawake na vijana kuanzisha miradi ya kiuchumi kwa njia ya mkopo midogo midogo,” amesema Mkurugenzi Mtendaji wa MWEA, Mary Sange.
Sange amesema hayo hivi karibuni katika kijiji cha Nyanchabakenye, wilaya ya Rorya koani Mara, wakati wa warsha iliyawakutanisha wanachama wa MWEA Tawi la Nyanchabakenye na timu ya viongozi kutoka Shirika la OIKOS lenye makao makuu yake jiijini Arusha.
“Lengo letu hapa ni kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusu maeneo ambayo tutashirikiana na MWEA,” amesema Mkurugenzi wa OIKOS, Mary Birdi.
Birdi amesema shirika lake hilo lina wataalamu waliobebea katika kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake na kwamba mafunzo hayo ni kipaumbele chao katika ushirikiano wao na MWEA.
Lakini pia Shirika la OIKOS litatoa mafunzo ya jinsia na haki za binadamu (gender and human rights) kwa wananchama hao wa MWEA.
“Shirika letu lilianzi mwaka 1999 na tumekijita kutoa mafunzo ya ujasiriamali, jinsia na haki za binadamu kwa wanachama wa MWEA,” amesema Birdi.
“Eneo linginge ambalo wataalamu kutoka OIKOS watajihusisha nalo ni kuwajengea uwezo (capacity building) wananchama hao katika kuendesha miradi ya kijamii (community grant, ameongeza Mkurugenzi huyo.
Sange amesema mafunzo ya jinsia na haki za binadamu yatakayotolewa na shirika la OIKOS ni muhimu kwa maendeleo endelevu ya shughuli za kiuchumi za wanachama hao.
“Unajua jamii yetu ina mfumo dume, lakini mume na mke wakipata mafunzo ya jinsia na haki za binadamu hata mikopo tunayowapa wanachama wa MWEA itakuwa salama,” amesema Sange.
Shirika la OIKOS pia limejikita katika kusaidia kuboresha huduma ya maji na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ambayo linafanya shughuli zake.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWEA, Sange, amesema ushirikiano wao na shirika la OIKOS unatarajiiwa kubadilisha maisha ya mamia ya wananchama wa MWEA katika vijiiji mbalimbali vilivyopo eneo la bonde la mto Mara nchini Tanzania.
Vijiji hivyo ni Buswahili, Ketasakwa, Nyamerambaro, Kwibuse, Surubu na Mara Sibora.
Vikundi takriban 12 vitawezeshwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kimazingira na kiuchumi katika vijiji hivyo chini ya uratibu wa MWEA, kwa mujibu wa Sange.
Sange ametaja miradi itakayoanzishwa kuwa ni ufugaji kuku, uzalishaji vitalu vya miche ya miti ya aina tofauti, kutengeneza machujio ya maji (water filters), malambo ya maji na ufugaji nyuki.
“Kila kijiji wamechagua mradi wao na lengo ni uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii kwa njia ya kipato na hii haitakuwa mikopo,” amesema Sange.
Christina Matiko ambaye ni mnufaika wa MWEA Tawi la Nyanchabakenye, amesema anaona mwanga mkubwa mbele yake kutokana na ujio wa OIKOS.
“Tayari nina miradi ya kiuchumi ambayo nimeanzisha baada ya kupata mkopo kutoka MWEA na sasa mafunzo tutakayopata yatatusadia kwenda vizuri zaidi,” Matiko ambaye ni Katibu wa Nidhamu katika Kikundi cha MWEA Tawi la Nyanchabakhenye amesema.
Kwa mujibu wa Sange, kwa sasa shirika la MWEA Tawi la Nyanchabhakenye lina wanachama 28 na hadi sasa limeshawafikia wanawake na viijana zaidi ya 10,000 katika wilaya za Musoma, Butiama, Bunda na Rorya tangu mwaka 2007 lilipoanzishwa.
(Imeandikwa na Mugini Jacob, Rorya)
No comments:
Post a Comment