NEWS

Sunday, 25 April 2021

Komote Mwenyekiti mpya wa ALAT Mkoa wa Mara

Mwenyekiti mpya wa ALAT Mkoa wa Mara, Daniel Komote

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote, amechaguliwa kwa asilimia 99 ya kura zote kuwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Mara, anafasi ambayo ataitumikia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Komote (aliyesimama) akiwashukuru wajumbe wa ALAT Mkoa wa Mara mara baada ya kumchagua kwa kishindo

Komote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nkende wilayani Tarime, amechaguliwa kushika madaraka hayo katika kikao cha kwanza cha wajumbe wa ALAT Mkoa wa Mara kilichofanyika mjini Musoma, Aprili 22, mwaka huu.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages