NEWS

Sunday 23 May 2021

Bodi ya Maji Bonde Ziwa Victoria yampongeza RC MalimaAdam Kighoma Malima

BODI ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) imemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Kighoma Malima aliyehamishiwa Mkoa wa Tanga, kwa mchango na ushirikiano mkubwa aliounesha katika usimamizi wa rasilimali za maji mkoani Mara.

“Kama RC uliweka jitihada katika kuhakikisha jamii na wadau wanashiriki ipasavyo kulinda na kutunza rasilimali hii muhimu. Tutaendelea kuthamini mchango wako na kuendeleza yote uliyoyafanya.

“Bodi inakutakia heri na fanaka katika majukumu yako mapya ya Ukuu wa Mkoa wa Tanga,” imeeleza taarifa ya LVBWB kupitia akaunti yake ya Instagram, leo Mei 23, 2021.

Wana-Mara wengi, wadau wa uhifadhi, utalii na uwekezaji watamkumbuka RC Malima pia kwa juhudi kubwa alizofanya katika kuhamasisha uhifadhi endelevu wa wanyamapori, mazingira, utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na mapori ya akiba, uwekezaji katika sekta za madini, kilimo na uvuvi mkoani Mara.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages