NEWS

Tuesday 25 May 2021

RC Gabriel awasili Mara, RAS aongoza mapokezi yake, kuzindua maonesho ya bidhaa, teknolojia na huduma mbalimbali



Mkuu mpya wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi.

MKUU mpya wa Mkoa (RC) wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi amewasili mkoani humo ambapo mapokezi yake rasmi yanaongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) huo, Caroline Mtapula mjini Musoma, leo Jumanne Mei 25, 2021.

Mapokezi hayo yanawashirikisha viongozi mbalimbali wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa na viongozi wa dini.

Mapema leo asubuhi RC Gabriel amezuri katika ofisi za CCM mkoa wa Mara  na kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya chama hicho tawala  .

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya RAS Mkoa wa Mara, kesho Jumatano Mei 26, 2021, RC Gabriel anazindua rasmi maonesho ya bidhaa, teknolojia na huduma mbalimbali katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma.


RAS Mkoa wa Mara, Caroline Mtapula.

Jana Jumatatu Mei 24, 2021, RAS Mtapula ameongoza kikao maalum cha maandalizi ya uzinduzi wa maonesho hayo na Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara.

Maonesho hayo yatafungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kabla ya kuzindua Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara Ijumaa Mei 28, 2021 kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex mjini Musoma.

MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

  1. Tupo tayari kuendana na mabadiliko na kasi atakayotaka mkuu wetu wa mkoa,Mungu amlinde vema

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages