NEWS

Wednesday 26 May 2021

RC Gabriel azindua maonesho ya bidhaa Mara, aahidi ushirkiano kwa mwekezaji wa kiwanda cha mafuta ya alizeti Rorya



RC Gabriel (kushoto) akipongeza uwekezaji wa kiwanda cha mafuta ya alizeti alipotembelea banda la bidhaa hizo mjini Musoma, leo.

MKUU mpya wa Mkoa (RC) wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, leo Jumatano Mei 26, 2021, amezindua rasmi maonesho ya bidhaa, teknolojia na huduma mbalimbali katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma.

RC Gabriel ambaye amefuatana na Katibu Tawala Mkoa (RAS) wa Mara, Caroline Mtapula, amepata fursa ya kutembelea mabanda ya maonesho na kujionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa mkoani humo.

Miongoni mwa mabanda ya maonesho ametembelea ni pamoja na la kiwanda cha mafuta ya alizeti cha Nyihita Sunflower kutoka wilayani Rorya.

Mkuu huyo wa mkoa amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa mwekezaji wa kiwanda hicho ambacho kimeanzishwa na mwekezaji mzawa.


Mfanyakazi wa kiwanda cha mafuta ya alizeti cha Nyihita Sunflower (kulia) akimweleza RC Gabriel namna wanavyojizatiti kuzalisha bidhaa hizo.

Kiwanda hicho tayari kimeanza kuzalisha mafuta ya kula (kupikia) huku kikikabiliwa na changamoto ya malighali kwa sasa.

“Mwekezaji huyu aungwe mkono na tusimwache mwenyewe,” RC Gabriel amesema akimwagiza Afisa Kilimo wa Mkoa wa Mara kufanyia kazi maelekezo hayo.


Wafanyakazi wa Northern Highlands Coffee Company wakionesha kahawa inayozalishwa na kampuni hiyo ikiwa kwenye vifungasho maalumu katika viwanja vya maonesho vya Mukendo mjini Musoma.

RC Gabriel amesema wawekezaji wanapaswa kupewa ushirikiaano na Serikali ili waweze kufikia malengo yao.

Afisa Elimu ya Huduma na Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara, Zake Rwiza akitoa maelezo ya huduma za mamlaka hiyo kwa mteja aliyetembelea banda lao katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma, leo.

Banda la TCCIA Mkoa wa Mara likiwa na bidhaa mbalimbali vikiwemo vinywaji aina ya KANROY kinachozalishwa na kampuni ya Karantini inayomilikiwa na mwekezaji mzawa wilayani Tarime.


RC Gabriel (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Serengeti Safari Marathon alipotembelea banda lao kwenye viwanja vya maonesho vya Mukendo mjini Musoma.

Maonenesho hayo yataendelea hadi Ijumaa Mei 28, 2021 ambapo kuhitimishwa kwake kutafanyika sambasmaba na uzinduzi wa Muongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mara.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Muongozo huo utakaofanyika kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex mjini Musoma, anatarajia kuwa Waziri MKuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages