NEWS

Tuesday, 4 November 2025

Dkt. Samia aapishwa kuwa Rais wa Tanzania muhula wa pili



Dkt. Samia Suluhu Hassan akila kiapo cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - mbele ya Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-------------

Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapishwa kuwa Rais wa Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – kwa muhula wa pili, katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma jana Jumatatu Novemba 3, 2025.

Rais Samia, mwenye umri wa miaka 65, alikula kiapo chake mbele ya Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, akiahidi "kulinda na kutetea Katiba na umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Dkt. Samia alitangazwa mshindi Jumamosi Novemba 1, 2025 kwa asilimia 97.66 ya kura zilizopigwa katika Uhaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Naye Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi aliapishwa katika hafla hiyo kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages