NEWS

Thursday 27 May 2021

C-Sema, ATFGM Masanga watoa elimu ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia



Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Itiryo wakicheza ngoma ya asili katika kongamano hilo.

WANAHARAKATI wa kutetea haki za binadamu na kupinga unyanyasaji wa kijinsia wamekemea ndoa za utotoni na vitendo vya ukeketaji kwa wasichana wilayani Tarime,badala ya kuwasomesha.

Wakizungumza katika kongamano la kutoa elimu ya kupinga ukeketaji kwa kutumia maandiko matakatifu lililoandaliwa na asasi ya C-Sema na Shirila la ATFGM Masanga Kanda ya Bwirege, wamesema kuwa katika dunia ya sasa vitendo hivyo havikubaliki.

Mkurugenzi wa huduma ya simu kwa watoto C-Sema, Michael Marwa ameitaka jamii ya watu wa Tarime Vijijini kuachana na mila ya kuwaoza watoto wakiwa wadogo, badala yake wawasomeshe kwani mtoto wa kike ndiye hukumbuka kwao.

“Somesheni mtoto wa kike kwa sababu anakumbuka nyumbani kuliko wa kiume, tuache kuwakeketa msiwashushe thamani, wasomesheni wawe madaktari, marubani na majaji badala ya kuwakeketa na kuwaoza wakiwa wadogo,” alisema Marwa.

Mnasihi wa kituo cha huduma kwa mtoto wa kike, Anastanzia Makasi amesema Shirika la C- Sema linatoa nafasi kwa watoto wa kike kuwapigia simu namba 116 na kuwaeleza changamoto zinazowakabili zikiwemo afya ya mama na mtoto.

Valerian Mgani ambaye ni Meneja Mradi wa ATFGM Masanga, amesema kongamano hilo la siku 12 linalenga kutoa elimu juu ya madhara yatokanayo na ukeketaji na ndoa za utotoni katika kanda ya Bwirege, Nyabasi na Renchoka. “Tumeamua kuandaa kongamano hili kwa ufadhili wa UNFPA ili kuwashirikisha viongozi wa dini watumie mandiko ya Quran na Biblia kutoa elimu hiyo kwa sababu wana watu wengi nyuma yao,” alisema Mgani.


Washiriki wa kongamano hilo wakifuatilia mafundisho

(Habari na picha: Mobini Sarya)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages