NEWS

Sunday 6 June 2021

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria, Nyasulugi waadhimisha Siku ya Mazingira kwa kupanda miti bonde la mto Mori


JUMUIYA ya watumia maji ya Nyasulugi iliyopo katika wilaya ya Rorya mkoani Mara, imeadhimisha Siku wa Mazingira Duniani mwaka huu kwa kupanda miti katika bonde la mto Mori.

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB), kupitia ofisi zake ya Dakio la Mara-Mori zilizipo Musoma, imeshirikiana na jumuiya hiyo kufanikisha upandaji miti katika kijiji cha Utegi, jana Ijumaa Juni 5, 2021.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga akipanda miti katika eneo la bonde la mto Mori, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Rorya, Simon Odunga ameshiriki pia katika shughuli hiyo na kupongeza jumuiya hiyo na LVBWB kwa kuendelea kuendelea kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.

Odunga ametumia fursa hiyo pia kukemeaa biashara ya mkaa ambayo inachangia kuharibu mazingira katika wilaya hiyo.

“Viongozi wasisite kuwachukulia hatua watu wote wanaochafua mazingira na vyanzo vya maji, maana madhara yake ni makubwa na tishio kwa vizazi vijavyo,” Mkuu huyo wa wilaya ameonya.

Amesema uchafuzi wa vyanzo vya maji huchangia milipuko ya magonjwa kama vile kichocho.

Miti 500 ilipandwa katika hafla hiyo, ambapo lengo la jumuiya hiyo ni kupanda miti milioni tatu katika vijiji 17, ikiwa ni sehumu ya juhudi zinazofanywa na wadau kurudisha uoto wa asili katika bode la mto Mori, kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Thomas Nkaina.

DC Odunga (kushoto) na Ofisa wa Dakio la Mara- Mori, Mhandisi Mwita Mataro (kulia) wakifurahi baada ya kukamilisha shughuli ya upandaji miti.

Nkaina amesema jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2019 kwa lengo la kutunza, kulinda rasilimali za maji na kutoa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji, hasa kuelewa madhara ya kulima na kujenga ndani ya mita 60 kutoka chanzo cha maji.

DC Odunga pia amepata nafasi ya kutembelea mabwawa ya samaki ambayo yako chini ya jumuiya hiyo na kujionea namna ufugaji huo unavyofanyika.


Wakiwa kwenye bwawa la kufugia samaki

Ofisa wa Dakio la Mara- Mori, Mhandisi Mwita Mataro ameshiriki pia katika shughuli hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa juhudu zinazofanywa na ofisi hiyo kuunga juhudi za LVBWB na jumuiya za watumia maji katika kulinda mazingira na vyanzo vya maji mkoani Mara, nyumbani kwa mto Mara upande wa Tanzania.
Mhandisi Mataro akipanda mti katika shughuli hiyo

Kwa mujibu wa Mhandisi  Mataro  ofisi yake imetoa miti 5,000 ambayo itapandwa katika vijiji 17 wilayani Rorya  ikiwa ni mwendelezo wa juhudi  zinafanywa na LVBWB kuhifadhi vyanzo vya maji  na mazingira kwa ujumla.

Siku ya Mazingira Duniani huadhimishwa Mei 5 kila mwaka kwa kauli mbiu ambazo zinalenga kutunza na kuhifadhi mazingira duniani ambapo kauli mbiu kwa mwaka huu 2021 ni : “Tutumie Nishati Mbadala Kuongoa Mfumo Ikolojia”.


Mto Mara na Mto Mori, yote inatiririsha maji yake katika Ziwa Victoria upande wa Tanzania.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages