NEWS

Sunday 6 June 2021

TB Joshua afariki dunia

TB Joshua

Taarifa iliyotolewa na kanisa lake la SCOAN siku ya Jumapili alfajiri imethibitisha kifo cha Muhubiri TB Joshua.

Muhubiri huyo maarufu kutoka nchini Nigeria amefariki akiwa na umri wa miaka 57.

Taarifa hiyo ilisema: Mungu amechukua maisha ya muhudumu wake TB Joshua kulingana na uwezo wake. Amefariki akimuhudumia Mungu.

Taarifa hiyo imetaja sura moja katika biblia inayosema : Mungu muweza hawezi kufanya lolote bila kutoa mipango yake kwa watume wako. " - Amos 3: 7.

Siku ya Jumamosi tarehe 5 Juni 2021, mtume TB Joshua alizungumza katika mkutano wa runinga ya Emmanuel.

''Kila kitu kina wakati wake - tunapokuja hapa na kuomba na tutarudi nyumbani baada ya utumwa''.

TB Joshua alikuwa mmoja wa wahubiri maarufu ambapo alijulikana kwa kutabiri matukio yajayo ambayo wengi waliona kama uingiliaji kazi ya Mungu.

Mwaka 2014, Muhubiri huyo alikosolewa nchini Nigeria baada ya upande mmoja wa paa la kanisa lake nchini humo kuanguka na kuwaua takriban watu 116.

Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

TB Joshua anajulikana kuwa muhubiri Mkristo anayehubiri katika runinga.

Ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambapo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.

TB Joshua ana makanisa mengi katika mataifa tofauti barani Afrika na Marekani ya kusini.


 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages