NEWS

Tuesday 22 June 2021

LHRC yakutanisha wadau kujadili sababu za migogoro wilayani TarimeKITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kupitia Mradi wa Jenga Amani Yetu, leo Juni 22, 2021 kimewakutanisha wadau wa asasi za kiraia na waandishi wa habari, kujadili vyanzo vya migogoro mbalimbali katika jamii wilayani Tarime, Mara.

Pia, wadau hao wamejadili kuhusu suluhusho la migogoro hiyo na namna ya kutumia fursa zilizopo kupata ruzuku zinazotolewa na mradi huo.


Wadau wakiendelea na majadiliano mkutanoni

Wadau walioshiriki mkutano huo mjini Tarime, ni waliokwishapata mafunzo maalum katika Mradi wa Jenga Amani Yetu, unaotekelezwa Tarime, Pwani, Tandahimba na Mtwara.

Pamoja na mambo mengine, wadau hao wamejadili migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, wanyamapori na binadamu, matatizo ya wizi wa mifugo, ukatili wa kijinsia, mfumo dume na watoto wa mitaani.


Picha ya pamoja

Akizungumza katika mkutano huo, Mratibu wa Mradi wa Jenga Amani Yetu, Caroline Shoo amesema mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa LHRC, SEARCH na ZLSC, kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages