NEWS

Thursday 17 June 2021

Kanisa la AICT lahimiza malezi bora kwa watoto



Watoto wakishiriki shindano la kusoma Siku ya Mtoto wa Afrika wilayani Tarime, Mara.

KANISA la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Mara na Ukerewe, limeitaka jamii kwa ujumla kushiriki katika kuwapa watoto haki zao za msingi ikiwemo kuwalinda, kuwasikiliza na kutowabagua katika elimu na masuala ya kiroho.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya kata ya Itiryo wilayani Tarime - Mara, Afisa Miradi wa kanisa hilo, Rebecca Zakayo Bugota amehimiza jamii kuzingatia mahitaji ya watoto.


Rebecca akizungumza katika maandhimisho hayo

“Kama kaulimbiu yetu ya mwaka huu inavyosema, “Tutekeleze Ajenda 2040: kwa Afrika Inayolinda Haki za Mtoto”, hivyo ni jukumu letu sisi sote kuendelea kumlinda mtoto na kumtunza,” amesema Rebecca.


Sehemu ya watoto walioshiriki maadhimisho hayo

Awali, akifungua maadhimisho hayo ambayo yaliandaliwa na Kanisa la AICT kwa kushirikiana na Taasisi ya Right to Play, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Elimu Kata ya Nyansincha, Sophia Range amekemea vitendo vya ukatili dhidi ya watoto katika jamii.


Sophia akihutubia maadhimisho hayo

Sophia amewataka wazazi waliojitokeza kwenye maadhimisho hayo kuwa chachu ya malezi, mafanikio na kukemea ukatili dhidi ya watoto ukiwemo ukeketaji kwa watoto wa kike.


Sophia akikabidhi zawadi kwa washindi

Maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto wa Afrika, a,mbayo hufanyika Juni 16 kila mwaka, yamefikia kileleni kwa mgeni rasmi kukabidhi zawadi kwa watoto walioweza kusoma vizuri na kwa washindi wa mpira, ambapo kombe lilienda kwa timu ya wasichana Itiryo, huku wanafunzi wa kiume kutoka Shule ya Msingi Nyonkoni wakiibuka na ushindi.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages