NEWS

Thursday 17 June 2021

Benki ya Exim yaahidi kuharakisha kibali cha kutekeleza mradi wa maji wa miji 28, baada ya kukutana na Waziri Aweso



Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (wa pili kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Nadhifa Kemikimba na watumishi wengine wa wizara hiyo kikaoni.

BENKI ya Exim ya India imeahidi kuharakisha utoaji wa kibali cha kukeleza mradi wa maji wa miji 28 nchini, baada ya uongozi wake kufanya kikao na Waziri wa Mji, Jumaa Aweso kwa njia ya kieletroniki, jana Juni 16, 2021.

Katika kikao hicho, Waziri Aweso amesisitiza uharakishwaji wa kibali hicho ili kazi za ujenzi wa mradi huo zianze.

Viongozi wa Benki ya Exim ya India wamekiri kuchelewa kutoa kibali hicho kutokana na mlipuko wa maradhi ya UVICO 19 katika nchi yao, hivyo kulazimisha kufanya kazi wakiwa nyumbani.


Kikao kikiendelea

Kikao hicho kimemalizika kwa viongozi wa Benki ya Exim ya India kukubali kuharakisha kutoa kibali ili kazi za ujenzi ziweze kuanza mara moja.

Mradi huo wa miji 28 una thamani ya Dola za Marekani milioni 500, ikiwa ni moja kati ya mradi mkubwa na wa kihistoria, utakaolemapinduzi makubwa katika sekta ya maji hapa Tanzania.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages