NEWS

Saturday 19 June 2021

Mbunge Ghati apiga jeki ujenzi wa ofisi za CCM Musoma Vijijini
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete ametoa msaada wa saruji mifuko 50 kuchangia ujenzi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM), unaendelea Musoma Vijijini.

“Nimefurahi sana leo kukabidhi mifuko ya saruji 50, ikiwa ni mchango wangu wa kusaidia ujenzi wa ofisi yetu ya CCM Musoma Vijijini,” Ghati amesema katika hafla ya kukabidhi saruji hiyo, jana Juni 18, 2021.


Mbunge Ghati (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa saruji mifuko 50 aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za CCM Musoma Vijijini. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Rhobi Samwelly.

Viongozi wa chama hicho tawala ngazi ya wilaya, wakiwemo madiwani wa viti maalum, wamepokea msaada huo na kumshukuru Mbunge Ghati kwa kuendelea kuwa mfano mzuri wa kuchangia maendeleo ya wananchi na chama hicho mkoani Mara.


Mbunge Ghati (anayenyanyua saruji kulia) akikabidhi msaada wa saruji mifuko 50 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za CCM Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UWT Taifa, Rhobi Samwelly na wa tatu kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa wa Mara, Sarah Kairanya.

Miongoni wa mwa viongozi waliohudhuria tukio hilo ni Katibu wa UWT Mkoa wa Mara, Sarah Kairanya na Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo Taifa, Rhobi Samwelly.


Viongozi mbalimbali wameshiriki katika tukio la makabidhiano ya msaada huo wa saruji.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages