NEWS

Monday 21 June 2021

RC Hapi awaapisha wakuu wa wilaya mkoani Mara
MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Salum Hapi, leo Jumatatu Juni 21, 2021 amewaapisha wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, juzi.

Walioapishwa na wilaya zao zikiwa kwenye mabano ni Joshua Nassari (Bunda), Dkt Vicent Mashinji (Serengeti, Juma Issa Chikoka (Rorya) na Mwalimu Moses Rudovick Kaegele (Butiama).


Mkuu mpya wa Wilaya ya Rorya, Juma Issa Chikoka (kulia) akila kiapo.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, RC Hapi amewataka wakuu hao wa wilaya kubuni vyanzo vya mapato na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao.
 
MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages