NEWS

Wednesday 16 June 2021

RUWASA yakanusha ubaguzi wa huduma ya maji Tarime




Mhandisi Malando Masheku

“TUNA shida kubwa sana ya maji, ingawa kuna watu wachache wapo maeneo yetu wao wanapata huduma ya maji,” amelalamika mwananchi, ambaye ni mtumishi wa Serikali mjini Tarime, Mara wakati akiongea na Mara Online News, jana.

Ofisi ya Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tarime, imekiri kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa huduma ya maji ya bomba kwa wakazi wa eneo la Kogete, kutokana na mioundombinu iliyopo kwa sasa, huku akikanusha uwepo wa ubaguzi wa huduma hiyo kwa wananchi wa eneo hilo.

“Tutajenga tenki jingine ambalo litasadia kusambazsa maji kwa wananchi wa Kogete na maeneo jirani kama Kebaga, kwa sababu miuondomibunu iliyopo kwa sasa haiwezi kupandisha maji. Hakuna ubaguzi pale,” Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tarime, Mhandisi Malando Masheku ameimbia Mara Online News ofisini kwa leo Juni 16, 2021.

Mhandisi Masheku amesema ofisi yake imeweka mradi wa Kogete kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022, ambayo utekelezaji wake utaanza Julai mwaka huu ili kuwawezesha wananchi 5,167 wa eneo hilo na maeneo jirani kupata huduma maji safi ya bomba.

“Sio Kogete tu, tutatekeleza miradi 12 katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tarime. Tumejipanga vizuri, haiwezekani watu wa vijijini wanapata maji safi, sisi mjini hatuna maji safi, tumejipanga,” amesisitiza Mhandisi huyo wa RUWASA.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages