NEWS

Tuesday 8 June 2021

Vijiji vyenye fursa ‘hot cake’ za utalii Tarime Vijijini



Hifadhi ya Taifa ya Serengeti - Eden ya Afrika

VIJIJI vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika wilaya ya Tarime mkoani Mara, viko kwenye maeneo ambayo unaweza kusema ni ‘hot cake’, yanayofaa kwa uwekezaji wa hoteli na kambi za kitalii.

Maeneo hayo hayajawahi kuwa na hoteli wala kambi ya kitalii tangu Hifadhi hiyo ianzishwe, zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Mara Online News imebaini kuwa wananchi wa vijiji hivyo wanahitaji elimu kuhusu umuhimu wa sekta ya utalii na fursa zilizopo ili waweze kutenga maeneo kwa ajili ya kuunda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ambayo itashawishi na kuvutia uwekezaji wa kitalii.

“Ukiwa katika vijiji vile unaona manthari nzuri sana ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na ni maeneo potential (nyenye fursa). Kama wananchi wangekubali kuanzisha WMA, wangenufaika sana na matunda ya uhifadhi na utalii,” Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Kanda ya Magharibi, Martin Loibooki ameiamabia Mara Oline News, ofisini kwake Bunda, hivi karibuni.


Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inavyoonekana ukiwa juu ya baadhi ya milima Tarime Vijijini

Loibooki amesema vijiji hivyo vimepakana na maeneo ya hifadhi yenye mvuto wa kipekee ndani ya hifadhi hiyo bora Afrika na kivutio kikubwa cha utalii duniani.

Tayari TANAPA imeanza kuhamasisha wananchi wa vijiji hivyo kuchangamkia fursa za utalii zilizopo katika maeneo yao, na umuhumu wa uhifadhi wa wanyamapori kwa maendeleo endelevu.

Baadhi ya viijiji hivyo ni Kegonga, Nyandage, Masanga, Gibasso, Kenyamosabi na Karakatonga.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages