NEWS

Monday 28 June 2021

Wapewa mafunzo ya kusajili watoto Serengeti
SERIKALI kupitia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imeendesha mafunzo ya usajili wa vizazi kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kwa maofisa watendaji wa kata na watumishi wa vituo vya tiba katika wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Mafunzo hayo yamefanyika jana Juni 28, 2021 kwenye ukumbi wa Kisare mjini Mugumu, ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa usajili wa watoto wenye umri huo, unaotekelezwa na serikali kupitia RITA, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) na wadau wa maendeleo.Mafunzo hayo yatafuatiwa na kampeni ya usajili itakayoanza leo Juni 29 hadi Julai 3, 2021.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Serengeti, Gasper Irigo amewataka maofisa waandikishaji hao kutekeleza mpango huo kwa weledi na kuhakikisha watoto wote ambao ni Watanzania waliopo Serengeti wanasajiliwa kwa ajili ya kupata vyeti vya kuzaliwa.Mafunzo hayo yameendeshwa na Mwezeshaji wa Kitaifa na Afisa Usajili kutoka RITA, Gaston Katindila na Mratibu wa Usajili Wilaya ya Serengeti, Maria Mlacha.

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti, Sunday Wambura ameipongeza RITA kwa kuandaa mafunzo hayo, na maofisa waliohudhuria kwa kuonesha utulivu na ufuatiliaji wa mada.

(Habari na picha: Emmanuel Mwita)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages