NEWS

Wednesday 28 July 2021

Diwani awaita wawekezaji kwenye chemichemi ya maji ya motoChemichemi ya maji ya moto wilayani Serengeti

DIWANI wa Majimoto wilayani Serengeti, Johannes Masirori ametoa wito kwa wawekezaji kutembelea katani hapo ili kujionea chemichemi ya maji ya moto na kufanya uwekezji wa kitalii.

“Tuna eneo linalotoa maji ya moto ardhini, jambo ambalo sio la kawaida… maji hayo yanaweza hata kuunguza mtu,” Masirori ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu, hivi karibuni.

Amesema uwekezaji katika eneo hilo utaiwezesha kata hiyo kuingiza mapato kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya wana-Majimoto.


Diwani Masirori akigusa chemichemi hiyo ya maji ya moto

“Tunapata wageni mbalimbali wanaokuja kuona kivutio hiki, lakini hatupati chochote, kuna kitu kinatakiwa kufanyika hapa,” Diwani Masirori amesema.

Ameongeza kuwa kuna uwezekano eneo hilo linalobubujisha maji ya moto, likawa na gesi pia.

(Imeandikwa na Mara Online News, Serengeti)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages