NEWS

Saturday 31 July 2021

Rorya wajibu mapigo utalii wa ndani Hifadhi ya Serengeti




WIKI moja baada ya kundi kubwa la watalii wa ndani kutoka wilaya ya Tarime kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kundi la watu zaidi ya 20, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa Benki ya NMB kutoka wilaya ya Rorya, wamejibu mapigo kwa kujitokeza kutembelea hifadhi hiyo.

Tayari watalii hao wa ndani kutoka Rorya, wameondoka leo Agosti 1, 2021 asubuhi kuelekea Hifadhi ya Serengeti.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB na familia zao kutoka wilaya ya Rorya wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Hoteli ya Goldland mjini Tarime, kabla ya kuanza safari kuelekea Hifadhi ya Serengeti, leo asubuhi.

Jumapili kama leo ya wiki iliyopita, watalii wa ndani 64 wa rika na jinsia tofauti kutoka Tarime, walitembelea hifadhi hiyo kupitia lango la Lamai, ambako walijionea mbashara vivutio mbalimbali, yakiwemo makundi ya wanyamapori kama vile nyumbu, tembo, kiboko, mamba, simba, twiga na swala.


Pamoja na wanyamapori wengine, watalii hao kutoka Rorya watashuhudia mbashara makundi ya nyumbu hawa, ambao hukaa Kaskazini mwa Hifadhi ya Serengeti kwa kipindi cha miezi minne, yaani Julai hadi Oktoba kila mwaka.

Safari hiyo ya watalii kutoka Rorya, ni mwendelezo wa mwitikio wa utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Lamai, unaohamasishwa na Mara Online kwa kushirikiana na Goldland Hotel & Tours na hifadhi hiyo.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni miongoni mwa vivutio bora na urithi wa dunia. Imepata Tuzo ya Hifadhi Bora Afrika kwa miaka miwili mfululizo, yaani 2019 na 2020. lakini pia imemilikishwa hadhi ya Maajabu Saba ya Dunia. Maelfu ya watalii kutoka mataifa mbalimbali humiminika kuitembelea hifadhi hii kwa ajili ya kujionea vivutio mbalimbali, yakiwemo makundi ya nyumbu wanaovuka Mto Mara kwenda Mbuga ya Maasai-Mara na kurudi Serengeti kila mwaka.


Hivi ndivyo nyumbu wanavyovuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages