
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akitangaza baraza jipya la mawaziri Ikulu Chamwino jijini Dodoma, leo Jumatatu Novemba 17, 2025.
Dodoma
------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza baraza jipya la mawaziri 27, ikiwa ni sehemu ya kurekebisha utendaji na kuongeza ufanisi ndani ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 17, 2025, Rais Samia amesema mabadiliko hayo yanahusisha kuanzishwa kwa wizara mpya, kubadilishwa kwa baadhi ya wizara za zamani na kuingizwa kwa sura mpya serikalini.
Miongoni mwa walioteuliwa kwa mara ya kwanza ni Dkt. Rhimo Nyansaho ambaye amepewa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na Joel Nanauka aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Wizara mpya Maendeleo ya Vijana itakayokuwa chini ya Ofisi ya Rais.
Rais Samia pia amewarejesha mawaziri kadhaa waliokuwa serikalini, akiwemo Prof. Adolph Mkenda, Jumaa Aweso, Prof. Makame Mbarawa na Profesa Paramagamba Kabudi.
Hata hivyo, baadhi ya mawaziri maarufu kama Hussein Bashe aliyekuwa akiongoza Wizara ya Kilimo, hawakurejea katika baraza jipya.
Pia, Dotto Biteko aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ameachwa kama ilivyo kwa Waziri wa muda mrefu, Jenista Mhagama (Afya) na Damas Ndumbaro (Katiba na Sheria).
Wengine waliotemwa ni Suleiman Jaffo (Viwanda na Biashara), Innocent Bashungwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Pindi Chana (Maliasili na Utalii).
Katika mabadiliko hayo, Rais Samia ametangaza kuanzishwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais, huku Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana ikibadilishwa kuwa Wizara ya Kazi, Ajira na Mahusiano, ambayo sasa itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Aidha, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ambayo kwa miaka mingi imekuwa chini ya Ofisi ya Rais, sasa imehamishiwa rasmi Ofisi ya Waziri Mkuu.
Ifuatayo ndiyo orodha kamili ya Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa:
1. Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Waziri: Ridhiwani Jakaya Kikwete
Naibu Waziri: Regina Ndege Qwaray
2. Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji
Waziri: Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Naibu Waziri: Pius Stephen Chaya
3. Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana- Waziri: Joel Arthur Nanauka
4. Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira
Waziri: Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
Naibu Waziri: Dkt. Festo John Dugange
5. Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu
Waziri: William Vangimembe Lukuvi
Naibu Waziri: Ummy Hamisi Nderiananga
6. Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano
Waziri: Deus Clement Sangu
Naibu Waziri: Rahma Riadh Kisuo
7. Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Waziri: Prof. Riziki Silas Shemdoe
Naibu Waziri (Elimu): Reuben Nhamanilo Kwagilwa
Naibu Waziri (Afya): Jafar Rajab Seif
8. Wizara ya Fedha
Waziri:Balozi Khamis Mussa Omar
Naibu Waziri: Laurent Deogratius Luswetula
Naibu Waziri: Mshamu Ali Munde
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri: Balozi Mahmoud Thabit Kombo
Naibu Waziri: Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe
Naibu Waziri: James Kinyasi Millya
10. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri: Boniface George Simbachawene
Naibu Waziri: Denis Lazaro Londo
11. Wizara ya Kilimo
Waziri: Mhe. Daniel Godfrey Chongolo
Naibu Waziri: Mhe. David Ernest Silinde
12. Wizara ya Maji
Waziri: Jumaa Hamidu Aweso
Naibu Waziri: Kundo Andrea Mathew
13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-Waziri: Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho
14. Wizara ya Ujenzi
Waziri: Abdallah Hamis Ulega
Naibu Waziri: Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya
15. Wizara ya Uchukuzi
Wazir:Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
Naibu Waziri: David Mwakiposa Kihenzile
16. Wizara ya Viwanda na Biashara
Waziri: Judith Salvio Kapinga
Naibu Waziri: Patrobas Paschal Katambi
17. Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Waziri: Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki
Naibu Waziri: Switbert Zacharia Mkama
18. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Waziri: Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima
Naibu Waziri: Maryprisca Winfried Mahundi
19. Wizara ya Afya
Waziri: Mohamed Omary Mchengerwa
Naibu Waziri: Dkt. Florence George Samizi
20. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Waziri: Prof. Adolf Faustine Mkenda
Naibu Waziri:Wanu Hafidh Ameir
21. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Waziri: Leonard Douglas Akwilapo
Naibu Waziri:Kaspar Kaspar Mmuya
22. Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri: Mhe. Ashatu Kachwamba Kijaji
Naibu Waziri: Hamad Hassan Chande
23. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Waziri: Prof. Palamagamba John Kabudi
Naibu Waziri: Hamisi Mwinjuma
Naibu Waziri:Paul Christian Makonda
24. Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Waziri: Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
Naibu Waziri: Mhe. Ng’wasi Damas Kamani
25. Wizara ya Madini
Waziri: Anthony Peter Mavunde
Naibu Waziri: Dkt. Steven Lemomo Kiruswa
26. Wizara ya Nishati
Waziri: Deogratius John Ndejembi
Naibu Waziri: Salome Wycliffe Makamba
27. Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri: Juma Zuberi Homera
Naibu Waziri: Zainabu Athman Katimba
No comments:
Post a Comment