NEWS

Sunday 1 August 2021

Watalii 550 kutoka Israel kuzuru Hifadhi za Taifa Tanzania




WATALII 550 kutoka nchi ya Israel wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa makundi na nyakati tofauti kuanzia kesho Agosti 2, 2021 kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Agosti 1, 2021, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano katika Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelutete amesema watalii hao watatembelea Hifadhi za Taifa zilizopo Kaskazini mwa Tanzania na Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Shelutete amesema kundi la kwanza lenye idadi ya watalii 150 litawasili nchini kwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kesho.


Pascal Shelutete

Amesema ujio wa watalii hao ni matunda ya juhudi kubwa za utangazaji utalii zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, sambamba na jitihada za makusudi zinazochukuliwa na serikali hiyo katika kukabiliana na UVIKO-19 (COVID-19) kwa miongozo inayoendelea kutolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ikiwemo kuhamasisha na kutoa chanjo ya ugonjwa huo.

“Aidha, kuwepo kwa ubalozi wa Tanzania nchini Israel nako kumechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la watalii kutoka nchini humo,” amesema Shelutete na kuongeza kuwa mwaka jana Tanzania ilipokea watalii zaidi ya 1,000 kutoka Israel waliokuja kutembelea vivutio mbalimbali na kwamba idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mwaka huu.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages