NEWS

Saturday 28 August 2021

Waziri Aweso ataka mageuzi sekta ya maji Handeni, CPA Msiru aanza kutekeleza agizo
BAADA ya Waziri ya Wa Maji, Jumaa Aweso (pichani juu wa pili kushoto) kukagua vyanzo vya maji na kutoa siku 30 kwa watendaji wa wizara hiyo kutatua kero ya maji katika wilaya ya Handeni, Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Wizara ya Maji, CPA Joyce Msiru na timu ya wataalamu wameingia kazini kuanza utetekelezaji wa agizo hilo.

Jana Agosti 27, 2021, CPA Msiru na timu ya watalamu wa wizara hiyo, wamekagua miundombuinu ya maji ili kupata mpango wa haraka wa kutatua kero ya maji kwa wananchi wa Handeni mkoani Tanga.


CPA Msiru (kushoto mbele) na wataalamu wakikagua miundombinu ya maji wilayani Handeni

Hali ya upatikanaji wa maji safi Handeni imeelezwa kutoridhisha, ambapo mmoja ya viongozi wa huko alilazimika kunywa maji yenye rangi ya tope mbele ya Waziri Aweso aliyekuwa katika ziara ya kikazi wilayani hapo.

Waziri Aweso naye alionja maji hayo, kabla ya kuwaagiza watendaji wake chini ya usimamizi wa CPA Msiru, kuweka mkakati mahususi wa kumaliza tatizo hilo ndani siku 30.


CPA Msiru (katikati) na wataalamu wakijadilianda jambo kuhusu mpango wa uboreshaji wa huduma ya maji wilayani Handeni.

“Nataka mageuzi wilaya ya Handeni. Joyce nakwambia tena sitaki mchezo Handeni, tafuta mtu ambaye atakuja kupambana hapa alete maji… alete maji Handeni mjini, maji yamwagike. Kazi unaiweza na ndio maana tukakuteua,” Waziri Aweso amemwagiza CPA Msiru mbele ya mkutano wa hadhara, baada ya kukagua vyanzo vya maji wilayani hapo.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages