NEWS

Saturday 28 August 2021

Mafundi Umeme watwaa kombe la Professor Mwera Foundation




TIMU ya soka Mafundi Umeme (pichani juu) imetwaa zawadi ya beberu la mbuzi, baada ya kuichapa Mafundi Mitambo na Magari kwa penati 5-3, katika mashindano ya Kombe la Professor Mwera Foundation (PMF).

Wachezaji na mashabiki wa timu ya Mafundi Umeme wakiwa wamembeba mchezaji aliyefunga bao la ushindi

Wachezaji wa timu ya Mafundi Mitambo na Magari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.

Nayo timu ya mpira wa wavu ya wasichana ya Waongoza Watalii imeinyuka timu ya Wasaidizi wa Maabara na kujinyakulia zawadi ya mbuzi.

Wachezaji wa timu ya Waongoza Watalii wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi.
Wachezji wa timu ya Wasaidizi wa Maabara katika picha ya pamoja na viongozi

Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya PMF kupitia chuo chake cha mafunzo ya ufundi cha Tarime Vocational Training College, na timu hizo zote zilizoshiriki jana Agosti 27, 2021 zinaundwa na wanafunzi wa chuo hicho.

Mgeni rasmi, Mwalimu Taabu (kushoto) akipokea mbuzi kutoka kwa Meneja wa Chuo hicho, Frank Joashi kwa ajili ya kukukabidhi kwa mshindi.

Mgeni rasmi akikabidhi zawadi

Mkurugenzi taasisi ya PMF, Hezbon Peter Mwera mbali na kutoa zawadi za mbuzi kwa washindi wa kwanza wa timu za mpira wa miguu na wavu, ametoa zawadi ya kreti tatu za soda kwa kila timu iliyoshika nafasi ya pili, kama pongezi ya kufika fainali.

Mgeni rasmi akiendelea kukabidhi zawadi

Mgeni rasmi katika mashindano hayo, Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Mwalimu Taabu Lazaro Majembe ameupongeza uongozi wa taasisi ya PMF, kwa kuanzisha mashindano hayo yanayolenga kutambua vipaji vya wanachuo hao.

Mkurugenzi wa taasisi ya PMF, Hezbon Peter Mwera (wa pili kushoto), mgeni rasmi, Mwalimu Taabu (wa pili kulia) na viongozi wengine wakifuatilia mashindano.

“Kwa kweli chuo hiki kimefanya jambo la msingi kuanzisha mashindano haya, ambayo yanaweza kutumika kumotisha watoto kusoma vizuri na kutambua vipaji vyao,” Mwalimu Taabu amesema.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages