MGENI Rasmi katika Uzinduzi wa Maadhimisho ya
Kumi ya Siku ya Mara, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Col. Michael
Mntenjele(aliyevaa kofia), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha
Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria, Perpetua Masaga.
|
MKUU wa
Wilaya ya Tarime, Col. Michael Mntenjele leo amezindua rasmi Maadhimisho ya
10 ya Siku ya Mara ambayo yanatarajiwa kufikia kilele Kesho. Uzinduzi
huo umefanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime, baada ya DC huyo
kutembelea mabanda ya mamlaka, taasisi na mashirika mbalimbali ya serikali na
binafsi kwenye viwanja hivyo. Mapema
leo asubuhi , DC Mntenjele aliongoza viongozi na wadau wa mazingira kutoka
ndani na nje ya Mkoa wa Mara, kupanda miti kando ya Mto Mara katika Vijiji vya
Mrito na Kerende. Amesema
jumla ya miti 15,000 imepandwa tangu juzi, jana na leo pamoja na Bicon
(Vigingi) 70 zimesimikwa ikiwa sehemu ya shughuli za maadhimisho hayo kwa Mwaka
huu. Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo anatarajiwa
kuw Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. Maadhimisho
ya kwanza ya Siku ya Mara yalifanyika mwaka 2012 nchini Kenya na kwa upande wa
Tanzania yalifanyika mwaka 2013 katika mji wa Mugumu, wilayani Serengeti. Kaulimbiu
ya maadhimisho hayo mwaka huu ni: "Tuhifadhi Mto Mara kwa Utalii na Uchumi
Endelevu",
|
No comments:
Post a Comment