NEWS

Monday 27 September 2021

Katibu Mkuu Eng. Sanga ataka ubunifu sekta ya maji



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (pichani juu kushoto), amewataka watendaji na wataalamu wa sekta ya maji, kutumia ubunifu katika kutoa huduma na kuepusha gharama zisizo za lazima.

Mhandisi Sanga ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji wa wataalamu wa sekta ya maji mkoani Mtwara, mwishoni mwa wiki.


Mhandisi Sanga (kushoto) akikagua mradi wa maji na kutoa maelekezo kwa mtaalamu.

Amesisitiza umuhimu wa kutumia usanifu wa miradi utakaowezesha huduma ya majisafi kuwafikia wananchi kwa njia ya mserereko na gharama ndogo.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages