NEWS

Monday 27 September 2021

Ushirika wa Mara watekeleza agizo la Waziri Mkuu Majaliwa
CHAMA cha Ushirika wa Wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMACU) kimeaza kutekelea agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu urejeshaji wa mali za ushirika zilizokuwa zimekabidhiwa serikali za mitaa na vijiji.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa WAMACU, Samwel Gisiboye, kazi za kubaini, kuhakiki na kurejesha mali hizo, zimeanza kuzaa matunda katika baadi ya maeneo ya mkoa huo.

“Mfano vijiji vya Nyangoto na Matongo vimekubali kurejesha mali zote na kuzikabidhi chini ya Ushirika,” Gisiboye amewambia waandishi wa habari mjini Tarime, hivi karibuni.

Ametaja baadhi ya mali hizo kuwa ni maghala, ardhi na kasiki.
Samwel Gisiboye
 
“Tunaishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri wanaotupatia, na hii ni kwa faida ya ushirika,” Gisiboye amesema.

Julai mwaka huu, Waziri Mkuu Majaliwa, aliagiza mali zote zirejeshwe kwenye Ushirika, ili kuuwezesha kuwa imara, bora na wenye tija kwa wakulima.

“Sisi tumeanza kutekeleza agizo hilo la Waziri Mkuu ambalo alilitoa katika maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani, yaliyofanyika Tabora Julai mwaka huu,” Gisiboye amesema.

Aidha, Serikali kupitia Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa, akishirikiana na Mrajis Msaidizi Mkoa wa Mara, wako mbioni kusaidia urejeshwaji wa mali za ushirika wa WAMACU zilizokuwa za MCU (1984) LTD, lilizopo chini ya Mfilisi.

Kwa sasa WAMACU inakusanya zao la kahawa kupitia Vyama vya Msingi vya Ushirika na Masoko (AMCOS).

Hivi karibuni, kimelipa malipo ya pili kiasi cha shilingi milioni 113 kwa wakulima waliouza kahawa aina ya Hard Arabica kwa chama hicho cha ushirika, msimu uliopita.

Kahawa safi

“Tulikusanya kahawa kwa bei ya shilingi 1,200 kwa kila kilo moja, lakini baada ya kuuza na kupata faida, tumewalipa wakulima malipo ya pili ya shilingi 400 kwa kila kilo moja.

“Tumetoa malipo hayo ya pili kwa sababu lengo la ushirika huu ni kuinua wakulima,” Gisiboye amesema.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages