NEWS

Wednesday 15 September 2021

Maadhimisho ya Siku ya Mara 2021 yafana Tanzania, Waziri Aweso atoa maagizo

Kwaya ya Wizara ya Maji ikitumbuiza katika Maadhimisho ya 10 ya Siku ya Mara 2021 wilayani Tarime, Tanzania, leo Septemba 15.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewahimiza wananchi kushirikiana na Serikali katika kutunza na kulinda hifadhi ya Bonde la Mto Mara, kwa maendeleo ya kiuchumi na ikolojia ya Serengeti.

“Maji ni uhai, maji ni maendeleo, maji ni kila kitu. Bonde la Mto Mara ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na ikolojia inayojumuisha Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

“Utunzaji wa Mto Mara ni jukumu la kila mtu. Utunzaji wa Mto Mara unaanza na wewe, mimi na sisi sote,” Waziri Awezo amesisitiza katika hotuba yake ya kuhitimisha Maadhimisho ya 10 ya Siku ya Mara 2021, kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime mkoani Mara, leo.

Waziri Awezo (aliyesimma) akihutubia umma

Waziri huyo amewataka wananchi kuepuka vitendo vya uharibifu na uchafuzi wa Mto Mara na bonde lake, ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji, kwa ajili ya mahitaji ya binadamu, mifugo, wanyamapori na mazingira kwa ujumla.

Waziri Aweso (kushoto) akipata maelezo ya shughuli za Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) zinazohusisha Mto Mara kwenye banda la maonesho ya bodi hiyo.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwaagiza viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya vijiji hadi mkoa, kuhakikisha shughuli za binadamu zinazoendeshwa ndani ya Bonde la Mto Mara, haziathiri kina na ubora wa maji ya mto huo.

Waziri Aweso (kulia) akisikiliza maelezo kwenye banda la maonesho ya Wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMACU).

“Tushirikiane na jamii katika kampeni ya uhifadhi, ulinzi na upandaji miti iliyo rafiki kwa vyanzo vya maji na rasilimali za maji,” Waziri Aweso amesisitiza.

Waziri huyo ametaja shughuli za binadamu zilizo rafiki kwa uhifadhi wa Bonde la Mto Mara katika vijiji jiraji kuwa ni pamoja na ufugaji wa kisasa na matumizi ya nishati ya gesi.

TarimeWaziri Aweso (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugezi wa Taasisi ya Professor Mwera Foundation, Hezbon Peter Mwera (kushoto) katika banda la maonesho ya shughuli za taasisi hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Col. Michael Mntenjele, amewataka viongozi wa vitongoji, vijiji, kata na tarafa kusimamia utunzaji wa miti iliyopandwa na vigingi vilivyosimikwa kwenye hifadhi ya Mto Mara kipindi hiki cha maadhimisho hayo ya mwaka huu, yenye kaulimbiu inayosema “Hifadhi Mto Mara kwa Utalii na Uchumi Endelevu.”


Afisa wa TFS Wilaya ya Tarime, Martin Ngongi (kulia) akimpatia mteja, Peter Madaha, maelezo ya kifaa cha kuchakata mazao ya nyuki wa asali aliyetembelea banda lao la maonesho.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages