NEWS

Sunday 17 October 2021

Mbunge Kembaki amwaga msaada wa jezi, mipira kwa timu 12 za soka Tarime Mjini
MBUNGE wa Tarime Mjini, Michael Kembaki ametoa msaada wa jezi na mipira kwa timu 12 za soka za jimbo hilo.

Hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo imefanyika katika uwanja wa mpira wa Serengeti mjini Tarime leo jioni hii ya Oktoba 17, 2021.

Katibu wa mbunge huyo, Elisha Samo amekabidhi vifaa hivyo kwa wahusika, akiwa amefuatana na afisa michezo wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Teddy Msiangi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Tarime, Malema Sollo.

Elish Samo (kulia) akikabidhi vifaa hivyo kwa wahusikaSamo amesema msaada huo ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na Mbunge Kembaki katika kundeleza sekta ya michezo ndani ya jimbo hilo.

Baadhi ya timu zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Magoma, Boss Ruge, Bomani, Thadeo, Kilimo Sports Club, Kenyamanyori na Nyamwigwira.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages