NEWS

Friday 8 October 2021

Mkurugenzi Kabaka ataja siri ya kuanza kupaa kwa mapato Butiama
MAKUSANYO ya mapato ya ndani katika Halmshauri ya Wilaya ya Butiama yameanza kuongezeka, baada ya usimamizi kuimarishwa, Mkurugenzi Mtendaji, Patricia Kabaka (pichani juu) amesema.

“Mfano Agosti mapato yetu yalikuwa shilingi milioni 87 na Septemba yaliongezeka hadi milioni 90,” DED Kabaka ameiambia Sauti ya Mara kwa nija ya simu, hivi karibuni.

Amewapongeza madiwani wa halmashauri hiyo kwa kuonesha ushirikiano mzuri katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani.

“Yaani sasa hivi madiwani wanasimamia wenyewe suala la ukusanyaji mapato na tumeimarisha usimamizi,” amesema.

Kabaka amesema watumishi wazembe katika ukusanyaji mapato wamewekwa pembeni na nafasi zao kuchukuliwa na wengine ili kuleta ufanisi.

“Vyanzo vyetu vikubwa [vya mapato ya ndani Butiama] ni masoko,” Kabaka amesema.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo amekanusha madai ya ubadhirifu wa fedha za umma katika halmashauri hiyo kwa sasa. “Butiama hali ni shwari na hakuna pesa ambayo imeliwa kwa sasa,” amesisitiza.

Butiama ni moja ya halmashauri za wilaya za mkoani Mara, ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuwa na vitendo vya ‘upigaji’ fedha za miradi ya maendeleo mara kwa mara.

(Na Mwandishi wa Mara Online News)

1 comment:

  1. Hongera sana mkurugenzi Patricia Rhobi Kabaka kwa usimamizi mzuri. Mwenyezi Mungu akusaidie katika kila hatua.

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages