NEWS

Thursday 7 October 2021

Kembaki apiga marufuku wajasiriamali kutozwa ushuru, aahidi milioni 10 ununuzi eneo la kujenga shule


MBUNGE wa Tarime Mjini, Michael Kembaki amepiga marufuku wajasiriamali kutozwa ushuru wa bidhaa wanazuza katika masoko ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Kembaki ametoa agizo hilo baada ya wajasiriamali wanaaouza ndizi na dagaa katika soko la Tarime kumweleza kero hiyo, alipowatembelea, leo Oktoba 7, 2021.

“Kuanzia leo natamka kwamba mkuu wa soko asitoze tena ushuru wowote, hadi pale kamati ya fedha na mipango ya halmashauri itakapokaa na kuamua vingenevyo,” amesema na kushangiliwa na wajasiriamali hao.

Mkuu wa soko hilo, Matiko Mang’era amejitetea kuwa ushuru huo unatokana na wadau kukaa na kuamua ili uweze kutumika kugharimia uzoaji taka sokoni hapo.

“Tulikaa na wadau wakakubaliana kwamba hawa akinamama wanaouza hapa sokoni wawe wanatozwa shilingi 200, lakini wale wanaosafirisha magunia walipie shilingi 500 bila kujali wingi wa magunia,” Mang’era amesema.

Katika hatua nyingine, Mbunge Kembaki ameahidi kutoa shilingi milioni 10 kuchangia ununuzi wa eneo la kujenga shule ya msingi katika mtaa wa Gimenya katani Turwa.


Mbunge Kembaki akikagua chanzo cha maji katika mtaa wa Gimenya.

Mwenyekiti wa mtaa huo, Nashon Samo amesema mitaa saba ilitakiwa kuchangia ununuzi huo, lakini mitatu imegoma na kwamba mwenye eneo hilo amekubali kuliuza kwa shilingi milioni 25.

“Nawachangia milioni 10, hapa naona panafaa, kwenye mitaa mingine eneo la nusu heka tu unaambiwa milioni sita, hapa ni zaya ekari nne, nampongeza huyu mwenye eneo ni mzalendo kweli kweli,” Mbunge Kembaki amesema.

(Na Mobini Sarya, Tarime)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages