NEWS

Thursday 21 October 2021

Serengeti yang'ara tena tuzo ya Hifadhi bora Afrika 2021.


Kwa mara nyingine, Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda Tuzo ya Hifadhi Bora Afrika kwa mwaka 2021, Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa mtandaoni leo  na Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA) kupitia mtando wake wa twitter.

"Kwa mara nyingine tena Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya Hifadhi Bora Barani Afrika kwa mwaka 2021" Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Masana Mwishawa, ameandika pia kwenye mtandao dakika chache zilizopita.

Ushindi huo unaifanya hifadhi hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania na yenye vivutio vya kipekee ikiwemo Simba, Tembo ,Nyati, Faru, Twiga, Chui na misafara ya makundi ya Nyumbu inayohama kutwaa tuzo hiyo kwa miaka mitatu mfululizo (1919, 2020 na 2021) ikizibwaga hifadhi zingine ikiwemo  Kruger ya Africa kusini.

Mara Online News itaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu tuzo hiyo kadiri itakavyozipata.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages