MBUNGE wa Jimbo la Tarime mjini, Michael Kembaki leo amekabidhi kisima cha asili ambacho amekiboresha ili kusaidia kuongeza huduma ya maji kwa wakazi wa mitaa miwili ndani ya mji huo ambao bado unakabiliwa na tatizo la huduma ya majisafi.
Mitaa itakayonufaika na huduma ya kisima hicho ni Mawasiliano na Bomani.
Mbunge kembaki akikagua utokaji wa maji katika kisima cha asili ambacho amekiboresha
“Wakati wa kampeni nilikuja hapa nikakutana na akinamama wakianiambia wakinipigia kura niwajengee kisima hicho, nikatoa ahadi ya kukijenga kisima hiki baada ya kuombwa kufanya hivyo na nimefurahi leo nimetimiza ahadi yangu”,Kembaki amesema leo jioni wakati akikabidhi kisima.
Katibu wa mbunge Kembaki, Elisha Samo akitoa maelezo ya mradi huo
Mbunge huyo ametumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuboresha kisima hicho ambacho alisema kikitunzwa vizuri kitasaidia na mitaa mingine jirani.
(Habari na Mobini Sarya, Tarime)
No comments:
Post a Comment