NEWS

Wednesday 6 October 2021

Mbunge Kembaki atimiza ahadi yake Shule ya Buhemba
MBUNGE wa Tarime Mjini, Michael Kembaki (pichani juu kulia) amekabidhi msaada wa mashine ya kisasa ya kuchapisha karatasi (printer) katika Shule ya Msingi ya Mazoezi Buhemba Mazoezi iliyopo kata ya Bomani.

Kembaki amekabidhi msaada huo kwa uongozi wa shule hiyo leo Oktoba 6, 2021 kutekeleza ahadi yake aliyoitoa wakati wa mahafali ya wahitimu wa darasa la saba mwaka huu.

Afisa Elimu Kata ya Bomani, Thabita Kesowani na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kordun Kivuyo wamemshukuru mbunge huyo na wakiahidi kuitumia vizuri kwa maendeleo ya shule.

“Kupitia printer hii, tunatarajia ufaulu kuongezeka maradufu na tunapenda kumhakikishia mbunge kuwa hata mtihani uliofanyika juzi, ufaulu utaongezeka,” Mwalimu Kivuyo ameiambia Mara Online News baada ya kupokea msaada huo.

Aidha, Mbunge Kembaki ameahidi kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 1,500.

(Na Mobini Sarya, Tarime Mjini)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages