NEWS

Friday 26 November 2021

Butiama, GRA-TZ wasaini MoU kunusuru mazingira

VIJIJI vya Mwikoro na Kigori katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama vimesaini makubalinao (MoU) na Shirika la Global Resources Alliance – Tanzania (GRA-TZ) ya kutekeleza mradi ambao utakaosadia kurejesha uoto wa asili katika vijiji hivyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa GR-TZ, Madaraka Nyerere amesema mbali na kurejeshwa wa uoto wa asili katika vilima, mradi huo utawezesha wananchi wa vijiji hivyo kuanzisha miradi ya kiuchumi ambayo ni rafiki kwa mazingira.

Madaraka amesema mradi huo wa miaka mitano unatakelezwa na GRA-TZ kwa kushirikiana na Shirika la WeForest lenye makao makuu Brussels nchini Ubeligiji.
DED Butiama Patricia Kabaka (kushoto) na Madaraka Nyerere wakisaini MoU ya mradi huo

“Manufaa makubwa ya mradi huu ni kuhifadhi vilima katika eneo la mradi na kuzuia sasa watu wasipande kwenye vilima kukata miti,” Madaraka ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, amesema leo Ijumaa Novemba 26, 2022 mara baada ya makubaliano hayo kusainiwa katika ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.
Madaraka na Meneja wa Mradi huo, Clavin Onesmo wakisaini

Kwa kuwa mradi huo pia unalenga kuzuia wananchi wasikate miti kwenye milima, utekekelezaji wake, Madaraka amesema utawezesha wananchi kuanzisha miradi mbadala ya kujipatia kipato, hususan ufugaji nyuki.

Utekelezaji wa mradi huo katika vijiji hivyo unatarajia  kuanza mapema mwakani.

Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Patricia Kabaka amesema mradi huo umekuja wakati ambao kuna tishio la mazingira katika wilaya hiyo kutokana na shughuli za kibinadamu, ikwemo ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

“Hali ya mazingira vijijini siyo nzuri na mradi utasaidia kuweka uhifadhi wa mazingira sawa,” DED Kabaka amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Peter Wanzagi Nyerere amesema usimamizi wa mradi huo utakuwa mkubwa.

“Kwanza hii ni neema kutoka kwa Mungu kupata mradi wa shirika la GRA na tutasimamia ili kuwa mfano, sio tu Butiama bali na nje ya wilaya ya Butiama,” Wanzagi amesema.

Meneja wa mradi huo kutoka GRA, Calvin Onesmo amesema utasaidia

kurejesha uto wa asili katika hekta 1,900 tayari kukabilina na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

“Pamoja na kurejesha uoto wa asili, mradi huu utajihusisha na miradi midogo midogo ya kukuza uchumi ngazi ya kaya, kama ufugaji wa nyuki, lakini pia utawezesha kupata hati miliki za kimila,” Onesmo amesema.

Hati miliki za kimila hizo ziatawasaidia hata kupata mikopo katika ngazi ya kaya na kuwekeza katika kilimo, amesema.

Suala la kilimo mseto litapewa pia kipaumbele wakati utekelezaji wa mradi huo, ambapo wananchi watawezeshwa kufanya hivyo, kwa mujibu wa Onesmo.

GRA-TZ ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) ambalo limejikita kusaidia uhifadhi wamazingira mkoani Mara, ikiwemo maoneo oevu ya mto Mara ambao ni mto wakimataifa na wenye umuhimu katika uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti namaisha ya watu zaidi ya milioni 1.1 katika mataifa ya Tanzania na Kenya.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages