NEWS

Tuesday, 23 November 2021

Milioni 60/- za UVIKO kunusuru mamia ya wanafunzi kusomea chini ya miti sekondari ya Kiriba Musoma Vijijini



Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo

WAKATI Shule ya Sekondari ya Kiriba iliyopo jimbo la Musoma Vijijini ikijiandaa kupokea wanafunzi 431 wa kidato cha kwanza, imepokea Sh milioni 60 kutoka serikalini, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa.

Fedha hizo ni sehemu ya bilioni 1.3 ambazo Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imepata mkopo kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwa ajili ya kupambana na janga la UVIKO-19 nchini.

“Bila fedha hizo, baadhi ya wanafunzi wa shule hii wangelazimika kusomea chini ya miti,” Taarifa kutoka ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini imesema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakazi wa kata ya Kiriba inayoundwa na vijiji vya Bwai Kumsoma, Bwai Kwitururu na Kiriba wamehamasika na kuamua kuchangia nguvu kazi kwenye ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati.

Pia, wanavijiji hao na wadau wao wa maendeleo, tayari wamekamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara kwa ajili ya masomo ya Fizikia, Kemia na Biolojia.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages