NEWS

Monday 1 November 2021

Ushirika wa Wakulima wa Mara kununua hisa za milioni 50 Benki ya Ushirika
CHAMA cha Ushirika wa Wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMACU), kimeamua kuwekaza kwenye Benki ya Ushirika (KCBL), ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mrajis wa Ushirika nchini, ili kuendeleza ushirika.

Mkutano Mkuu wa WAMAKU uliofanyika mjini Tarime Oktoba 29, 2021, ulipitisha mpango wa ununuzi wa hisa 100,000 kwenye KBCL, zenye thamani ya shilingi milioni 50.


Mwenyekiti wa Bodi ya WAMACU, David Hechei (kushoto) akizungumza katika mkutano huo.

Agizo la Mrajis wa Ushirika nchini, kupitia barua yake ya Oktoba 12, 2021, linavitaka vyama vyote vya ushirika kuwekeza kwenye benki hiyo.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa WAMACU, Samwel Kisiboye, bei ya ununuzi wa hisa moja kwenye KCBL ni shilingi 500 na kiwango cha chini kinachotakiwa kwa kila chama cha ushirika ni shilingi 200,000 sawa na hisa 400.

“Chama kinaweza kuwekeza zaidi kutokana na uwezo wake,” Kisiboye amesema.

Meneja Kisiboye akizungumza na Mara Online News ofisini kwake.

Mwenyekiti wa Bodi ya WAMACU, David Hechei amewahimiza wajumbe wa mkutano huo kuwekeza kwenye ununuzi wa hisa za KBCL, kukata bima, kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na kuendelea kuzalisha kahawa yenye ubora ili waweze kunufaika zaidi.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages