NEWS

Wednesday 15 December 2021

Gari la DC Rorya lapata ajali
GARI la Mkuu wa Wilaya (DC) ya Rorya, Juma Issa Chikoka limetapa ajali na kusababisha majeraha kwa devera wake.

Taarifa zilizoifikia Mara Online News zinasema ajali hiyo imetokea eneo Ingiri Juu wilayani humo leo Desemba 15, 2021 ambapo gari lililohusika ni lenye namba za usajili STL 2412

Gari hilo limepata ajali wakati likienda kumfuata DC Chikoka nyumbani kumpeleka ofisini kwake, majira ya saa mbili asubuhi.

“DC hakuwemo kwenye gari, alikwemo dereva ambaye amejeruhiwa na amekimbizwa katika hospitali ya Shirati kupata matibabu,” kiMEsema chanzo chetu cha uhakika kutoka serikalini.


DC Chikoka amezungumza na Mara Online News kwa njia ya simu, lakini hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia ajali hiyo.

“Hello, nipo kwenye kikao nitafute baadaye, nitafute baade," Chikoka amesema kwa ufupi.

#MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages