NEWS

Monday 13 December 2021

CCM Tarime wakagua ujenzi vyumba vya madarasa, Mwenyekiti Ngicho aridhishwa kasi ya utekelezaji

CCM Tarime wakagua ujenzi vyumba vya madarasa, Mwenye
kiti Ngicho aridhishwa na kasi ya utekelezaji

MWENYEKITI wa chama tawala - CCM Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Marwa Daudi Ngicho jana Desemba 13, 2021 ameongoza wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya hiyo kukagua miradi ya maendeleo, ukiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Viongozi wengine waliofuatana na Ngicho katika ziara hiyo ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Valentine Maganga, Mwenyekiti wa Halmashauriya Mji wa Tarime, Daniel Komote na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Simion Kiles maarufu kwa jina la K.

Miradi ya ujenzi wa vyumba vya madasara na ofisi za walimu iliyokaguliwa ni ambayo inatekelezwa kutokana na mabilioni ya fedha yaliyotolewa na IMF kama mkopo kwa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kampeni ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Baadhi ya shule hizo ni Turwa,, Bomani, Nyandoto, Nkende, Nyamisangura, Kenyamanyori, Nkongore na Kitare.

Ngicho ameeleza  kufurahishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi  hiyo.

“Nimefurahishwa na hatua ambazo shule nyingi zimefikia katika ujenzi wa vyumba na madarasa, maana kwa asilimia 76 naona ujenzi unaendelea vizuri," bosi huyo wa CCM wilayani Tarime amesema.

Wakuu wa shule zilizopata miradi hiyo, wametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaptia mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuitekeleza.

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia pesa, sasa mamia ya wanafunzi watapata elimu bila shida," amesema Mwalimu Chacha Nchagwa ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari mpya ya Turwa.

Viongozi hao wanandelea na ziara katika maeneo mengine ya wilaya hiyo leo

(Habari na picha zote: Geofrey John Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages