NEWS

Sunday 12 December 2021

Kituo cha Afya Mugini Polyclinic chazinduliwa TarimeKITUO cha afya cha kisasa cha Mugini Polyclinic kimezinduliwa rasmi katika mji wa Tarime mkoani Mara, kwa ajili ya kutoa huduma bora za matibabu.

Kituo hicho kimezinduliwa na Paroko wa Parokia ya Tarime, Padre Lucas Chacha, ambapo kabla ya kukizindua rasmi Desemba 11, 2021, ameongoza ibada fupi ya kumshukuru Mungu.


Paroko Chacha (kushoto) akiwa amekata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo hicho. Anayeshangilia ni Mkurugenzi Mugini.

Baadaye katika hotuba yake, Paroko Chacha amempongeza Mkurungezi wa kituo hicho cha afya, Gabriel Mugini kwa kuona umuhimu wa kuanzisha huduma hiyo mjini Tarime.

Paroko huyo ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha wataalamu wa afya wa kituo hicho kuhudumia wagonjwa kwa upendo, umakini na weledi.

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Simon K. Samwel, Paroko Chacha, Mkurugenzi Mugini na mke wake.


Naye Mkurugenzi Mugini amesema ana kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kumjaalia kuanzisha kituo hicho cha afya.

“Tumejipanga kutoa huduma bora za matibabu na afya kwa ujumla kwa wananchi ndani na nje ya Tarime, kwa gharama rafiki,” Mkurugenzi Mugini amesema.

Ameongeza “Tumejipanga vizuri sana, watumishi waliopo ni waliobobea, lakini pia kituo hiki cha afya kimekidhi mahitaji muhimu na vigezo vyote vinavyotakiwa. Huduma zinazopatikana hapa ni sawa na zinazopatikana Musoma, Mwanza na Dar es Salaam.”
Mkurugenzi Mugini na mke wake

Mkurugenzi Mugini amesema kituo hicho cha afya kina maabara ya kisasa inayopima kila aina ya ugonjwa.

(Habari na picha zote: Yohana Gitano wa Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages