NEWS

Saturday 11 December 2021

Eng Kemikimba, CPA Msiru wakagua miradi ya maji MaraNAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba (pichani juu kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Masingira Wizara hiyo, CPA Joyce Msiru (kushoto) wapo katika ziara ya kikazi mkoani Mara, kukagua miradi ya maji ili kuhakikisha inatekelezwa kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Viongozi hao jana wamekagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji Mugango-Kiabakari, utasaidia kusambaza huduma ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kwa wa maelefu ya wananchi wa halmashauri za wilaya za Butiama na Musoma Vijijini.

Utekelezaji wa mradi huo utagharimu shilingi bilioni 70.5, kwa mujibu wa Wizara ya Maji.


Hapa wakipata maelezo kutoka kwa watekelezaji wa mradi huo

“Maendeleo ya utekelezaji wa mradi yanaridhisha na hata ujenzi wa tenki umefikia asilimia 98,” Mmoja wa viongozi hao ameileza Mara Online News, leo asubuhi.

Leo, viongozi hao wanatarajia kukagua ujenzi wa chujio la maji katika mradi mwingine mkubwa wilayani Bunda.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages