MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote amehimiza wananchi kujenga utamaduni wa kuhudhuria mikutano ya mitaa yao ili kujua mipango ya maendeleo yanayowahusu.
"Wananchi mliopo hapa naomba mfikishe ujumbe huu kwa wenzenu, hii ndo maana halisi ya Serikali kushirikisha wananchi, sasa nyie kama hamji kwenye vikao tutawashirikishaje?" Komote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nkende amesema katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo mjini Tarime, leo Desemba 6, 2021.
Komote akihutubia kikao hicho
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19, lakini pia kutoa ushirikiano kwenye sensa ya watu na makazi ijayo.
Madiwani kikaoni
Viongozi wa kisiasa na Serikali kikaoni
Wakati huo huo, Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Tarime, limekumbusha kuwa hadi sasa gharama ambayo mwananchi anapaswa kulipa ili kuunganishiwa huduma ya umeme nyumbani ni Sh 27,000.
(Habari na picha zote: Asteria John wa Mara Online News)
No comments:
Post a Comment